|  | 
| Naibu wa chansela Prof Erastus Njoka amkabidhi Francis makucha | 
Tuesday, November 20, 2018
 Chuo cha Chuka chawafanyia Fadhila walemavu
Wanasema waswahili kwamba Dau la mnyonge haliendi joshi, na likienda litazama. Naibu wa chansela hakukubali kuliona dau la mwanafuni Francis Wanyama likizama. Ndipo akaamua kumfanyia francis fadhila kwa kumtunuku makucha mapya {crutches} kwani aliyokuwa akiyatumia yalikuwa yamechakaa. Kuterema kwa wanyama hakungefichika kwani alivaa tabasamu isiyo elezeka alipokuwa akikabidhiwa makucha yale. Chuo kikuu cha chuka kimelivalia njuga swala la kuwajali na kuwakubali wanafunzi na wafanyikazi walio na ulemavu. Chuo cha Chuka kimehakikisha kwamba wanafunzi hawa wanatamba na kutambaa katika majengo yake yote. Pamoja na hili, kitengo cha ushauri nasaha kimehakikisha kwamba unyanyapaa haupo miongoni ma wanafunzi wengine kwa kuwahamasisha umuhimu wa kuwakubali na kuwapenda wenzao waliolemaa. Aidha, prof. Erastus Njoka alitoa wito kwa jamii kuwapa elimu ya kutosha walemavu kwani wanauwezo na maarifa kama watu wengine wasio na ulemavu.
Chuo Cha Chuka chainuka
 Chuo Cha Chuka cha wavutia walio na tamaa ya kupata elimu
Chuo kikuu cha Chuka Kinaendelea kuinuka kwa kasi ya
kuduwaza. Chuo hiki ni mojawapo ya vyuo ambavyo vilianzishwa chini ya miaka
kimi na tano {15] iiyopita. Hata hivyo, kuongezeka ka idadi ya wanafunzi kadri
miaka inavyo songa kutoka wanafunzi mia tano{500} chuo kilipoanza , hadi
wanafunzi elfu kumi na saba {17000} sasa hivi ni dhihirisho tosha kwamba Chuo
hiki kinaingia katika orodha ya vyuo vya kimataifa. Aidha, usimamizi wa Chuo
cha Chuka ukiongozwa na Naibu wa Chansela Prof Erastus Nyaga Njoka unajizatiti
kujenga mijengo ya kisasa ambayo itaendana na hadhi na viwango vya juu vya
elimu chuoni humo. Miongoni mwa majengo hayo ni pamoja na Bweni la wanafunzi wa
kiume, kituo cha utafiti cha kisasa na umbo au jengo tawala ambalo linatazamiwa kuwa
kivutio kikubwa na uti wa mgongo wa chuo hicho. Bila shaka ni Dhahiri kwamba
Chuo Cha Chuka kinaenziwa na wengi na kitaendelea kuwavutia wengi walio na ari
ya kukifu kiu ya elimu na maarifa.
| Bweni la wanafunzi wa kiume | 
| Umbo Tawala litakalo kuwa kivutio kikuu chuoni Chuka{administration block} | 
Wanafunzi wa chuo cha Chuka Wachagua Viongozi
o
Baada ya muda wa kampeni na ahadi kochokocho kama ilivyo ada ya wanasiasa, siku ya kuwapima mizana wawaniaji wa nafasi tofauti iliwadia. Kwa kuwa chuo hiki kina vitivo 5 wawakilishi 15 wa wanafunzi hususan watatu kutoka kila kitivo mnamo januari 26 mwaka huu walijitosa katika uga wa pavilion kuwachagua viongozi.
Kwa kuwa chuo kikuu cha chuka kina enzi demokrasia, wanafunzi walipata fursa ya kuwania nafasi tofauti za uongozi katika chama cha wanafunzi .{Chuka University Students A ssociation}.
Uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa tofauti kwani bunge la kitaifa lilibatilisha mfumo wa awali ambapo wanafunzi waliruhusiwa kuwachagua viongozi moja kwa moja, hadi mfumo wa wawakilishi wa vitivo tofauti kuwachagua viongozi kwa niaba ya wanafunzi.
Shughuli nzima ya uchaguzi iliendelea bila bighudha yoyoyte ikizingatiwa kwamba chuo kilikuwa kimewaalika maafisa wa tume ya uchaguzi nchini ili kuendesha mpango huu pamoja na vitengo vya usalama vilivyokuwa vimeshika doria
Baadhi ya walio ibuka washindi ni pamoja na Livan Njeru, mwenye kiti,james kamau, katibu mkuu, paul ogeto, mweka hazina, moureen nyambura, katibu mwandaliza, john Momanyi, mwelekezi wa masomo na Josphat Maru, mwelekezi wa ustawi wa wanafunzi. Viongozi hawa walichukua rasmi jukumu la kilisukuma gurudumu la kuhakikisha ustawi wa wanafunzi umeshughulikiwa kwa kina.
“Hatuku kumbana na changamoto zozote za utovu wa nidhamu kama ilivyo kawaida ya chaguzi za vyuo vingine zinazo kumbwa na fujo na uharibifu wa mali.” Daktari Geodfrey Gathongo ambaye ni mwenye kiti wa tume ya uchaguzi alidokeza. Akishadidida haya, Joyce Macharia ambaye ni naibu wa mwamini wa ustawi aliwapongeza wanafunzi wote kwa nidhamu na utulivu unaoendelea kukipa chuo cha Chuka haiba na turuhani zisizo na kifani.
Katibu Mkuu
Mwenye Kiti
Kikundi cha wasakata densi cha New Blyden cha Chuka kilipata nafasi ya kuonyesha umahiri wao katika densi kwenywe kipindi maarufu sana nchini kenya{Churchil Show Meru Edition} baada ya kuibuka washindi kati ya vikundi ishirini. Kikundi hiki kilizinduliwa mwaka wa 2015 ambapo kilikuwa na wanachama watanonpeke yake. Kusudio la waanzilishi lilikuwa kuimarisha talanta sio tu katika densi bali pia sarakasi, michezo ya kuigiza na pia vichekesho. Bali na hayo New Blyden wamebobea kwa Sanaa licha ya changamoto nyingi kama vile kukosa ufadhili wa kifedha ili kuendeleza shughuli zao za kuimarisha talanta katika densi. Sasa hivi, New Blyden ni nyumbani kwa burudani kwa takriban wanafunzi nia moja ambao husakata densi katika warsha mbalimbali chuoni Chuka na pia sherehe zingine kama vile harusi.” Densi ina manufaa mengi kwani inawawezesha wengi kukifu mahitaji yao na hata kuanzisha biashara kutokana na malipo wanayo yapata baada ya kuburudisha hadhira. Aidha densi pia inamwezesha mwanafunzi kuepukana na tabia kama vile u;languzi wa dawa za kulevya , uasherati na pia kuweka dau almaarufu {Kamari}. “alidoke Nicholus Muriki mwenye kiti wa kikundi hiki. New Blyden wanatoa shukrani za dhati kwake Joyce Macharia ambaye ni naibu mwamini wa wanafunzi kwa juhudi zake kuhakikisha kwamba kikundi hiki kimepata fursa ya kuburudisha katika sherehe za chuo cha Chuka
Subscribe to:
Comments (Atom)
 




